YouVersion Logo
Search Icon

Plan Info

Soma Biblia Kila Siku 03/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 03/2024

DAY 6 OF 31

Yesu alifanya suluhu kwa dhambi zetu (2:17, Ilimpasa kufafanishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake ). Kwa hiyo Wakristo waitwa watakatifu (m.1), kwa kuwa walipokea msamaha wa dhambi kwa njia ya kumwamini. Ni watoto wa Mungu aliye mtakatifu. Waisraeli waliitwa taifa au nyumba ya Mungu, kwa kulishika agano la kale lililowafikia kupitia Musa (Hes 12:7, Mtumishi wangu, Musa, yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote ). Yesu ni mkuu kuliko Musa, kama agano jipya lilivyo kuu kuliko agano la kale. Katika Agano Jipya neno linawaelekeza watoto wa Mungu kwa Yesu, ambaye kwa yeye tumefanywa washiriki wa mwito wa mbinguni.

Scripture

Day 5Day 7

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 03/2024

Soma Biblia Kila Siku 03/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha ...

More

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy