YouVersion Logo
Search Icon

Plan Info

Soma Biblia Kila Siku 04/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 04/2024

DAY 4 OF 30

Ni maelezo juu ya maana ya tendo la ishara la Hosea katika ml.1. Uhusiano wa Mungu na Israeli ni kama ndoa iliyovunjika kwa sababu ya uzinzi wa “mama” (Ufalme wa Kaskazini). Uzinzi wake ni upi? Tafakari m.5 na 13 ambapo “wapenzi” ni mfano wa miungu: Mama yao amezini; yeye aliyewachukua mimba ametenda mambo ya aibu; maana alisema, Nitafuatana na wapenzi wangu, wanipao chakula changu na maji yangu, sufu yangu na kitani yangu, mafuta yangu na vileo vyangu. ... Nami nitamwadhibu kwa sababu ya siku za Mabaali, aliowafukizia uvumba; hapo alipojipamba kwa pete masikioni mwake, na kwa vito asema Bwana . Ilikuwa haki ya mke kupewa nguo na chakula na mume wake (Kut 21:10, Kwamba ajitwalia mke mwingine, chakula chake huyo, na nguo zake, na ngono yake, hatampunguzia ). Kwa sababu Israeli si mke wake tena, Mungu atamvua nguo zake na kuharibu mazao ya nchi yake. Ila angalia, Mungu anasema hivyo kwa sababu anawapenda Waisraeli na kutaka wamrudie. Inaonekana katika m.7 ilipoandikwa kuhusu Israeli, Atawafuata wapenzi wake, lakini hatawapata; atawatafuta, lakini hatawaona; ndipo atakaposema, Nitakwenda nikamrudie mume wangu wa kwanza; kwa maana hali yangu ya zamani ilikuwa njema kuliko hali yangu ya sasa.

Scripture

Day 3Day 5

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 04/2024

Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hos...

More

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy