YouVersion Logo
Search Icon

Plan Info

Soma Biblia Kila Siku 04/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 04/2024

DAY 1 OF 30

Siku hii ya pili ya sikukuu ya Pasaka ni siku ya kutembea na Yesu aliyefufuka. Sikukuu hii huambatana na utume wa Kristo Yesu anayewatuma akiwapa mamlaka wanafunzi kwenda kuipeleka Injili. Katika m.21 anawaambia, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi . Kama alivyotangaza amani kwa waliokuwa na hofu baada ya kifo chake, hata siku hizi Yesu bado anatangaza amani kwa watu wote, hata kwa wale wanaolemewa na mizigo ya dhambi. Leo Yesu anajifunua kwako kwa kupitia Neno lake, akisema, Njoni kwangu, ninyi nyote msumbuakao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha (Mt 11:28). Fungua moyo wako ili aingie na kufanya matengenezo moyoni mwako.

Scripture

Day 2

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 04/2024

Soma Biblia Kila Siku 04/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa nne pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Hos...

More

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy